Alhamisi, 4 Juni 2015

HISTORIA YA UBUNGE JIMBO LA KWIMBA


1. MUSOBI MAGENI MUSOBI
Mwenyekiti wa CUF awamu ya pili (1995 – 1999),
 aliyejiunga na chama cha wananchi CUF mwaka 1994
amefariki akiwa na umri wa miaka 81, amezaliwa April 01, 1931,

·        Wakati wa uhai wake alipata elimu ya Msingi katika Shule ya Kakola wilayani Kwimba, na baadae alipata elimu ya kati na Sekondari Dole iliyopo Zanzibar. Baada ya hapo 1950 alirudi wilayani Kwimba na mwaka mmoja baadae 1951 alipata kazi ya ukarani (Area Secretary) katika Halmashuri ya Maswa, na baadae 1954 akahamia Halmashauri ya Kwimba kama Muhasibu na mnamo 1957 akahamishiwa ukarani tena katika Halmashauri hiyohiyo ya Kwimba hadi 1961 alipoacha kazi na kufanya shughuli za ukulima.

·         Ilipofika mwaka 1965 aliamua kugombea ubunge jimbo la Mwamashimba wilaya ya Kwimba, alifanikiwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa awamu mbili hadi mwaka 1975, wakati huo akiwa mbunge alifanikiwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo Mijini mwaka 1972 na aliutumikia hadi 1975, kabla hajateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Chunya mwaka 1978, wilaya ya Kahama 1983 na wilaya ya Muleba 1988 hadi 1990.
Kitaaluma, pamoja na mafunzo ya Uhasibu na Ukarani, lakini pia alibahatika kupata mafunzo ya Uandishi wa Habari katika chuo cha Cambrige University mwaka 1968 na Chuo cha Social Training Centre cha Nyegezi, mkoani Mwanza.

2. MASANJA FRANCIS NCHIMANI (1975-1985)

** hakuna taarifa sahihi juu ya mhusika

3.  BALOZI GEORGE NHIGULA (1985-1995)


-Alikuwa mbunge wa jimbo la kwimba (1985-1995) kwa tiketi ya CCM kipindi cha mfumo wa chama kimoja
·        Kabla ya kuwa mbunge hayati balozi aliwahi kufanya kazi serikalini kwenye nyazifa tofauti
       i.            Katibu Mkuu wa kwanza mwafrika katika Wizara ya Kazi (1965-1966).
     ii.             Aliwahi kuwa balozi wa Tanzania katika nchi za Misri (1968-1971), Uingereza (1971-1974), Japan (1974-1978) na India (1978-1980). Pia, aliwahi kuwa Ofisa mwandamizi katika ubalozi wa Tanzania Marekani na alihusika kuanzisha ubalozi wa Tanzania nchini Sweden.

4. BUJIKU PHILIP SAKILA (1995-2010)



-Alikuwa mbunge wa jimbo la kwimba kwa tiketi ya CCM
ELIMU
·        Alikuwa na shahada ya elimu(BSc (Edu)) aliyoipata kwenye chuo kikuu cha UDSM
Mheshimiwa sakila aliwahi kufanya kazi serikalini kama ifuatavyo
       i.            Mwalimu wa sekondari kati ya mwaka (1974-1993), kabla ya kuwa mwalimu mkuu msaidizi mwaka (1993-1994). Na baadae kuwa mkuu wa shule (1994-1995)
     ii.            Naibu waziri wa elimu na utamaduni (1997-2005)

5. SHANIF HIRAN MANSOOR (2010- mpaka sasa)
 


-Ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi jimbo la kwimba kwa tiketi ya CCM
ELIMU
·        Mheshimiwa ana elimu ya sekondari (o-level education) aliyosoma mwaka 1982-1985
NAFASI ZA UONGOZI ALIZOPITIA
       i.            Afisa mtendaji mkuu(C.E.O) wa kampuni ya Mansoor Industries ltd kuanzia mwaka (1998- mpaka sasa)
     ii.            Mwenyekiti wa kampuni la Petroleum  Importation Coodinator ltd  kuanzia mwaka (sept 2011- mpaka sasa)

6. LETICIA MAGENI NYERERE (2010- Mpaka sasa)


-Ni mbunge wa viti maalum wa kuteuliwa (CHADEMA)
ELIMU
·        Masters of arts in finance (MA(finance))  aliyoisoma Corllins University, USA mwaka 2009-2011
KAZI NYINGINE ALIZOWAHI KUFANYA
Jina la kampuni                                           Nafasi                                       Mwaka
First Premier Mortgage
Senior Mortgage Consultant
2006
2010
Master Security Inc., Washington DC, USA
Security Screener for Federal Government Employees
2001
2005
Marshall Heights Community Development Organization, Inc., Washington, DC
Accounting Technician, Fraud Detector
1999
2001
International Commercial Services Ltd, Dar Es Salaam, Tanzania
Executive Director
1985
1999
International Commercial Services Ltd, Dar Es Salaam, Tanzania
Founder &Publisher of FEMINA Women Magazine
1985
1999
Bowie State University, Maryland, USA
Independent Lecturer (Women & Politics)
-
-











Vyanzo vya taarifa




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni